1  Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana. 
Psaumes 103.1  Psaumes 104.35  Psaumes 103.22-104.1  Psaumes 105.45  
 2  Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai. 
Psaumes 104.33  Psaumes 63.4  Psaumes 71.14-71.15  Psaumes 145.1-145.2  Apocalypse 7.9-7.17  
 3  Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. 
Psaumes 118.8-118.9  Esaïe 2.22  Jérémie 17.5-17.6  Psaumes 60.11  Psaumes 62.9  
 4  Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea. 
Psaumes 104.29  Ecclésiaste 12.7  Genèse 2.7  1 Corinthiens 2.6  Genèse 3.19  
 5  Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake, 
Psaumes 71.5  Psaumes 144.15  Jérémie 17.7-17.8  Exode 3.6  Psaumes 33.12  
 6  Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele, 
Apocalypse 14.7  Colossiens 1.16  Hébreux 6.18  Psaumes 100.5  Psaumes 117.2  
 7  Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa; 
Psaumes 68.6  Psaumes 103.6  Esaïe 61.1  Psaumes 145.15-145.16  Psaumes 12.5  
 8  Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki; 
Matthieu 9.30  Psaumes 145.14  Psaumes 11.7  Psaumes 147.6  2 Corinthiens 7.6  
 9  Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha. 
Psaumes 68.5  Jérémie 49.11  Psaumes 147.6  1 Corinthiens 3.19  Malachie 3.5  
 10  Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya. 
Psaumes 10.16  Exode 15.18  Esaïe 40.9  Daniel 7.14  Psaumes 145.13