Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 14.1
Bible en Swahili de l’est


1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.Psaumes 10.4 Romains 3.10-3.12 Genèse 6.11-6.12 Ephésiens 2.1-2.3 Romains 1.21-1.32
2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Psaumes 33.13-33.14 Genèse 6.12 Romains 3.11 Hébreux 11.6 2 Chroniques 19.3
3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.Romains 3.10-3.12 Job 14.4 Esaïe 53.6 Esaïe 59.13-59.15 Esaïe 64.6
4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana.Jérémie 10.25 Psaumes 79.6 Esaïe 64.7 Amos 8.4 Psaumes 27.2
5 Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.Psaumes 73.15 Psaumes 24.6 Psaumes 112.2 Psaumes 46.11 Psaumes 22.30
6 Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake.Psaumes 9.9 Psaumes 4.2 Psaumes 42.10 Hébreux 6.18 Matthieu 27.40-27.43
7 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.Psaumes 53.6 Psaumes 85.1

Cette Bible est dans le domaine public.