Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 138.4
Bible en Swahili de l’est


1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.Psaumes 111.1 Psaumes 95.3 Psaumes 119.46 Jean 10.34-10.36 Actes 23.5
2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.Psaumes 5.7 Matthieu 5.18 Matthieu 24.35 1 Rois 8.29-8.30 Esaïe 42.21
3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.Psaumes 18.6 Philippiens 4.13 Ephésiens 3.16 Colossiens 1.11 2 Corinthiens 12.8-12.10
4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.Psaumes 102.15 Psaumes 22.22 Psaumes 22.27 Psaumes 72.11 Esaïe 60.3-60.5
5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.Psaumes 21.5 Apocalypse 4.11 Malachie 1.11 Esaïe 52.7-52.10 Matthieu 21.5-21.9
6 Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.Proverbes 3.34 Jacques 4.6 Esaïe 57.15 Psaumes 113.5-113.6 Luc 1.48
7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa.Psaumes 71.20-71.21 Psaumes 23.3-23.4 Esaïe 5.25 Esaïe 41.10 Psaumes 85.6
8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.Philippiens 1.6 Psaumes 57.2 1 Thessaloniciens 5.24 Esaïe 26.12 Psaumes 136.1

Cette Bible est dans le domaine public.