1  Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. 
Exode 13.3  Psaumes 81.5  Genèse 42.23  Esaïe 11.16  Exode 12.41-12.42  
 2  Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. 
Lévitique 11.45  Exode 29.45-29.46  Exode 25.8  Ezéchiel 37.26-37.28  2 Corinthiens 6.16-6.17  
 3  Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. 
Psaumes 77.16  Exode 14.21  Josué 3.13-3.16  Psaumes 106.9  Habakuk 3.15  
 4  Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. 
Exode 19.18  Habakuk 3.6  Juges 5.4-5.5  Nahum 1.5  Jérémie 4.23-4.24  
 5  Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma? 
Habakuk 3.8  Jérémie 47.6-47.7  
 6  Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo? 
Psaumes 29.6  Psaumes 114.4  
 7  Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo. 
Psaumes 96.9  Esaïe 64.1-64.3  Psaumes 77.18  Psaumes 104.32  Job 26.11  
 8  Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi. 
Psaumes 107.35  Nombres 20.11  Deutéronome 8.15  Psaumes 105.41  Exode 17.6