Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 26.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!Job 16.4-16.5 Job 12.2 1 Rois 18.27 Job 4.3-4.4 Esaïe 35.3-35.4
3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!Actes 20.20 Actes 20.27 Job 33.33 Job 13.5 Job 15.8-15.10
4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?1 Rois 22.23-22.24 1 Jean 4.1-4.3 Job 32.18 Ecclésiaste 12.7 Job 20.3
5 Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao.Psaumes 88.10 Genèse 6.4 Job 41.1-41.34 Ezéchiel 29.3-29.5 Psaumes 104.25-104.26
6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko.Proverbes 15.11 Psaumes 139.8 Amos 9.2 Job 28.22 Hébreux 4.13
7 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.Job 9.8 Psaumes 104.2-104.5 Genèse 1.1-1.2 Esaïe 40.22 Esaïe 40.26
8 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.Proverbes 30.4 Jérémie 10.13 Esaïe 5.6 Job 38.37 Job 38.9
9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake.Psaumes 97.2 1 Timothée 6.16 Exode 20.21 Habakuk 3.3-3.5 Exode 33.20-33.23
10 Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.Proverbes 8.29 Job 38.8-38.11 Psaumes 33.7 Jérémie 5.22 Psaumes 104.6-104.9
11 Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake.1 Samuel 2.8 Apocalypse 20.11 Aggée 2.21 Job 15.15 Psaumes 18.7
12 Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake.Esaïe 51.15 Jérémie 31.35 Psaumes 89.9-89.10 Esaïe 51.9 Job 9.13
13 Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.Esaïe 27.1 Genèse 1.2 Psaumes 74.13-74.14 Psaumes 104.30 Psaumes 33.6-33.7
14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?Psaumes 29.3 Job 11.7-11.9 1 Corinthiens 13.9-13.12 Psaumes 139.6 Job 40.9

Cette Bible est dans le domaine public.