Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 20.1
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. 2 Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. 3 Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. 4 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. 5 Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote. 6 Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. 7 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. 8 Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. 9 Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.

Cette Bible est dans le domaine public.