Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 1.1
Bible en Swahili de l’est


1 Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.Romains 1.7 2 Thessaloniciens 1.1 Actes 18.5 2 Corinthiens 1.19 1 Pierre 5.12
2 Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.Romains 1.8-1.9 Philémon 1.4 Philippiens 1.3-1.4 Ephésiens 1.15-1.16 Colossiens 1.3
3 Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.1 Corinthiens 13.13 2 Thessaloniciens 1.11 Galates 5.6 Apocalypse 2.19 Romains 8.24-8.25
4 Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;2 Thessaloniciens 2.13 2 Pierre 1.10 Tite 3.4-3.5 1 Thessaloniciens 1.3 Ephésiens 2.4-2.5
5 ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.2 Thessaloniciens 2.14 Colossiens 2.2 1 Pierre 1.12 1 Corinthiens 12.7-12.11 2 Corinthiens 4.1-4.3
6 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.Actes 13.52 1 Corinthiens 11.1 Galates 5.22 1 Corinthiens 4.16 Actes 17.5-17.10
7 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.Tite 2.7 1 Timothée 4.12 1 Pierre 5.3 2 Corinthiens 9.2 2 Corinthiens 1.1
8 Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.Romains 1.8 2 Thessaloniciens 3.1 2 Thessaloniciens 1.4 Romains 16.19 Esaïe 66.19
9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;1 Timothée 4.10 Galates 4.8-4.9 1 Corinthiens 12.2 Actes 14.15 Osée 1.10
10 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.1 Thessaloniciens 5.9 Matthieu 3.7 Actes 2.24 Romains 4.25 Actes 1.11

Cette Bible est dans le domaine public.