Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 15.5
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.Nombres 21.28 Ezéchiel 25.8-25.11 Esaïe 11.14 Amos 2.1-2.3 Esaïe 14.28
2 Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.Lévitique 21.5 Jérémie 48.1 Esaïe 3.24 Deutéronome 34.1 Nombres 21.30
3 Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.Jonas 3.6-3.8 Esaïe 15.2 Jérémie 48.38-48.39 Esaïe 22.1 2 Rois 6.30
4 Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.Jérémie 48.34 Deutéronome 2.32 Esaïe 16.8-16.9 Nombres 32.3-32.4 Jonas 4.8
5 Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.Jérémie 48.5 Jérémie 4.20 Jérémie 9.18-9.19 2 Samuel 15.30 Genèse 13.10
6 Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.Nombres 32.36 Joël 1.10-1.12 Esaïe 16.9-16.10 Apocalypse 8.7 Nombres 32.3
7 Kwa hiyo vitu walivyojipatia tele, na akiba yao, wanavichukua hata kijito cha mierebi.Jérémie 48.36 Psaumes 137.1-137.2 Nahum 2.12-2.13 Esaïe 10.6 Esaïe 30.6
8 Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.Jérémie 48.20-48.24 Ezéchiel 47.10 Jérémie 48.31-48.34 Esaïe 15.2-15.5
9 Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninaweka tayari msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.2 Rois 17.25 Lévitique 26.21-26.22 Lévitique 26.28 Jérémie 50.17 Jérémie 15.3

Cette Bible est dans le domaine public.