Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Cantique 8.11
Bible en Swahili de l’est


1 Laiti ungekuwa kama ndugu yangu, Aliyeyanyonya matiti ya mamangu! Kama ningekukuta huko nje, Ningekubusu, asinidharau mtu.Galates 4.26 Zacharie 9.9 Esaïe 7.14 Luc 2.38 Esaïe 66.11-66.12
2 Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha; Ningekunywesha divai iliyokolea,Divai mpya ya mkomamanga wangu.Cantique 3.4 Cantique 7.12 Cantique 4.10-5.1 Galates 4.26 Jean 5.46-5.47
3 Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu, Nao wa kuume ungenikumbatia.Cantique 2.6 Esaïe 62.4-62.5 2 Corinthiens 12.9 Deutéronome 33.27
4 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha, Hata yatakapoona vema?Cantique 2.7 Cantique 3.5
5 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Akimtegemea mpendwa wake? Nalikuamsha chini ya huo mpera; Huko mama yako alikuonea utungu, Aliona utungu aliyekuzaa.Cantique 3.6 Cantique 2.3 Esaïe 40.3 Cantique 3.4 Cantique 6.10
6 Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.Esaïe 49.16 Aggée 2.23 Proverbes 6.34 Jérémie 22.24 Apocalypse 12.11
7 Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.Proverbes 6.35 Romains 13.8-13.10 Esaïe 43.2 Proverbes 6.31 Romains 8.28-8.39
8 Kwetu sisi tuna umbu mdogo, Wala hana maziwa; Tumfanyieje umbu letu, Siku atakapoposwa?Ezéchiel 16.55-16.56 1 Pierre 2.12 Psaumes 2.8 Ezéchiel 16.46 Luc 19.44
9 Kama akiwa tu ukuta, Tumjengee buruji za fedha; Na kama akiwa ni mlango, Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.Actes 15.16 Zacharie 6.12-6.15 1 Corinthiens 3.10-3.12 Esaïe 60.17 Esaïe 61.4
10 Mimi nalikuwa ukuta, Na maziwa yangu kama minara; Ndipo nikawa machoni pake Kama mtu aliyeipata amani.Ezéchiel 16.7 Genèse 6.8 Esaïe 60.10 Cantique 4.5 Cantique 7.7-7.8
11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomi Akawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu; Kila mtu atoe vipande elfu vya fedha kwa matunda yake.Ecclésiaste 2.4 Esaïe 7.23 Cantique 1.6 Esaïe 5.1-5.7 Cantique 7.12
12 Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, li mbele yangu. Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako, Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.Cantique 1.6 1 Timothée 5.17-5.18 1 Corinthiens 6.20 1 Timothée 4.15-4.16 Actes 20.28
13 Wewe ukaaye bustanini, Hao rafiki huisikiliza sauti yako; Unisikizishe mimi.Cantique 1.7 Cantique 6.11 Cantique 3.7-3.11 Cantique 5.9-5.16 Psaumes 45.14
14 Ukimbie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya manukato.Cantique 2.17 Apocalypse 22.17 Cantique 2.9 Apocalypse 22.20 Luc 19.12

Cette Bible est dans le domaine public.