1  Hekima umeijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; 
Ephésiens 2.20-2.22  Galates 2.9  1 Corinthiens 3.9-3.15  Matthieu 16.18  Hébreux 3.3-3.6  
 2  Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. 
Matthieu 22.3-22.14  Esaïe 25.6  Cantique 8.2  Proverbes 23.30  Genèse 43.16  
 3  Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, 
Proverbes 9.14  Proverbes 8.1-8.3  Psaumes 68.11  Romains 10.15  Jean 18.20  
 4  Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, 
Proverbes 6.32  Proverbes 9.16  Matthieu 11.25  Proverbes 8.5  Apocalypse 3.17-3.18  
 5  Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya. 
Jean 6.27  Cantique 5.1  Psaumes 22.26  Jérémie 31.12-31.14  Jean 6.49-6.58  
 6  Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. 
Proverbes 13.20  Proverbes 4.14-4.15  Proverbes 4.11  Proverbes 8.35  Actes 2.40  
 7  Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. 
2 Chroniques 24.20-24.22  1 Rois 21.20  2 Chroniques 36.16  Genèse 19.8-19.9  Proverbes 23.9  
 8  Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. 
Psaumes 141.5  Matthieu 7.6  Proverbes 29.1  Proverbes 13.18  1 Rois 1.23  
 9  Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; 
Proverbes 1.5  Matthieu 13.11-13.12  2 Pierre 3.18  Osée 6.3  1 Jean 5.13  
 10  Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. 
Proverbes 1.7  Job 28.28  Psaumes 111.10  Ecclésiaste 12.13  Proverbes 30.3  
 11  Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. 
Proverbes 3.16  Proverbes 10.27  Proverbes 3.2  Deutéronome 6.2  
 12  Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako. 
Job 22.2-22.3  Job 22.21  Esaïe 28.22  Job 35.6-35.7  2 Pierre 3.16  
 13  Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu. 
Proverbes 7.11  Proverbes 5.6  Proverbes 21.9  1 Timothée 6.4  Proverbes 21.19  
 14  Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka, 
Proverbes 9.3  Proverbes 7.10-7.12  
 15  Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao. 
Proverbes 7.25-7.27  Proverbes 7.13-7.15  Proverbes 23.27-23.28  
 16  Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, 
Proverbes 9.4  
 17  Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza. 
Proverbes 20.17  Proverbes 23.31-23.32  Proverbes 30.20  Proverbes 7.18-7.20  Ephésiens 5.12  
 18  Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni. 
Proverbes 7.27  Proverbes 1.7  Proverbes 6.26  Proverbes 2.18-2.19  2 Pierre 3.5