1  Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. 
Exode 15.6  Esaïe 52.10  Psaumes 96.1  Psaumes 96.3  Psaumes 33.3  
 2  Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. 
Esaïe 52.10  Esaïe 62.2  Esaïe 49.6  Romains 1.17  Marc 16.15  
 3  Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. 
Psaumes 22.27  Luc 1.72  Deutéronome 4.31  Luc 1.54-1.55  Romains 10.12  
 4  Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. 
Esaïe 44.23  Psaumes 66.1  Apocalypse 19.6  Psaumes 100.1  Psaumes 47.1-47.5  
 5  Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. 
Esaïe 51.3  1 Chroniques 15.16  Psaumes 33.2  Apocalypse 5.8  Apocalypse 14.2-14.3  
 6  Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. 
Apocalypse 19.16  2 Chroniques 29.27  2 Chroniques 15.14  Matthieu 25.34  2 Chroniques 5.12-5.13  
 7  Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. 
Psaumes 96.11-97.1  Psaumes 24.1  Esaïe 49.13  Esaïe 61.11  
 8  Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. 
Esaïe 55.12  Psaumes 47.1  Psaumes 89.12  Psaumes 93.3  2 Rois 11.12  
 9  Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili. 
Psaumes 96.10  Psaumes 96.13  Esaïe 5.16  Apocalypse 1.7  Romains 2.5-2.6