Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 98.3
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.Exode 15.6 Psaumes 96.1 Esaïe 52.10 Psaumes 96.3 Psaumes 33.3
2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.Esaïe 52.10 Esaïe 62.2 Esaïe 49.6 Psaumes 24.5 Jérémie 23.6
3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.Psaumes 22.27 Deutéronome 4.31 Luc 1.72 Psaumes 106.45 Romains 15.8-15.9
4 Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.Esaïe 44.23 Psaumes 66.1 Apocalypse 19.6 Psaumes 100.1 Psaumes 47.1-47.5
5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi.Esaïe 51.3 Apocalypse 14.2-14.3 2 Chroniques 29.25 Psaumes 92.3-92.4 1 Chroniques 25.1-25.6
6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.2 Chroniques 5.12-5.13 1 Chroniques 15.28 Psaumes 81.2-81.4 Nombres 10.1-10.10 Psaumes 47.5-47.7
7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.Psaumes 96.11-97.1 Psaumes 24.1 Esaïe 49.13 Esaïe 61.11
8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha.Esaïe 55.12 Psaumes 89.12 Psaumes 93.3 2 Rois 11.12 Psaumes 65.12-65.13
9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.Psaumes 96.13 Psaumes 96.10 Psaumes 67.4 Actes 24.25 Psaumes 72.2

Cette Bible est dans le domaine public.