Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 95.11
Bible en Swahili de l’est


1 Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.2 Samuel 22.47 Psaumes 89.26 Psaumes 81.1 Psaumes 107.8 Psaumes 117.1
2 Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.Psaumes 100.4 Ephésiens 5.19 Jacques 5.13 Psaumes 105.2 Psaumes 17.13
3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.Psaumes 97.9 Psaumes 96.4 Psaumes 145.3 Psaumes 135.5 Psaumes 48.1-48.2
4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake.Psaumes 135.6 Psaumes 21.2 Michée 1.4 Job 11.10 Habakuk 3.10
5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu.Genèse 1.9-1.10 Proverbes 8.29 Job 38.10-38.11 Jonas 1.9 Jérémie 5.22
6 Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.Psaumes 100.3 2 Chroniques 6.13 Daniel 6.10 Philippiens 2.10 Exode 20.5
7 Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!Hébreux 4.7 Hébreux 3.7-3.11 Hébreux 3.15 Psaumes 48.14 Psaumes 74.1
8 Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani.Exode 17.7 Nombres 20.13 Deutéronome 6.16 Exode 17.2 1 Samuel 6.6
9 Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.Nombres 14.22 1 Corinthiens 10.9 Psaumes 78.56 Psaumes 78.40-78.41 Psaumes 78.17-78.18
10 Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.Hébreux 3.17 Actes 7.36 Proverbes 1.22-1.29 Jean 3.19-3.21 Deutéronome 2.14-2.16
11 Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu.Nombres 14.23 Hébreux 4.3 Hébreux 4.5 Hébreux 3.18 Hébreux 3.11

Cette Bible est dans le domaine public.