Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 88.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.Luc 18.7 Psaumes 22.2 Psaumes 51.14 Psaumes 27.9 1 Chroniques 2.6
2 Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako.Psaumes 141.1-141.2 Psaumes 79.11 1 Rois 8.31 Lamentations 3.8 Psaumes 31.2
3 Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu.Psaumes 107.18 Job 6.2-6.4 Psaumes 107.26 Job 33.22 Psaumes 22.11-22.21
4 Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.Psaumes 28.1 Psaumes 143.7 Psaumes 30.9 Psaumes 109.22-109.24 Ezéchiel 26.20
5 Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako.Esaïe 53.8 Psaumes 31.22 Psaumes 88.16 Job 11.10 Psaumes 31.12
6 Mimi umenilaza katika shimo la chini, Katika mahali penye giza vilindini.Psaumes 69.15 Psaumes 143.3 Psaumes 86.13 Lamentations 3.2 Jude 1.13
7 Ghadhabu yako imenilemea, Umenitesa kwa mawimbi yako yote.Psaumes 42.7 Job 10.16 Romains 2.5-2.9 Psaumes 102.10 Jean 3.36
8 Wanijuao umewatenga nami; Umenifanya kuwa chukizo kwao; Nimefungwa wala siwezi kutoka.Psaumes 31.11 Esaïe 49.7 Zacharie 11.8 Jérémie 32.2 Psaumes 143.4
9 Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso Bwana, nimekuita kila siku; Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.Job 11.13 Psaumes 143.6 Psaumes 86.3 Psaumes 38.10 Jean 11.35
10 Wafu je! Utawafanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?Psaumes 6.5 Psaumes 30.9 1 Corinthiens 15.52-15.57 Esaïe 26.19 Marc 5.35-5.36
11 Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu?Psaumes 73.18 Matthieu 7.13 Proverbes 15.11 2 Pierre 2.1 Job 26.6
12 Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?Ecclésiaste 9.5 Ecclésiaste 2.16 Jude 1.13 Job 10.21-10.22 Matthieu 8.12
13 Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.Psaumes 5.3 Psaumes 30.2 Marc 1.35 Psaumes 119.147-119.148
14 Bwana, kwa nini kuitupa nafsi yangu, Na kunificha uso wako?Job 13.24 Psaumes 13.1 Psaumes 43.2 Psaumes 44.24 Psaumes 77.7-77.9
15 Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana, Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.Job 6.4 Job 17.11-17.16 Esaïe 53.3 Zacharie 13.7 Psaumes 22.14-22.15
16 Hasira zako kali zimepita juu yangu, Maogofyo yako yameniangamiza.Psaumes 90.11 Esaïe 53.8 Psaumes 89.46 Psaumes 102.10 Psaumes 90.7
17 Yamenizunguka kama maji mchana kutwa, Yamenisonga yote pamoja.Psaumes 22.16 Psaumes 118.10-118.12 Psaumes 42.7 Job 30.14-30.15 Job 16.12-16.13
18 Mpenzi na rafiki umewatenga nami, Nao wanijuao wamo gizani.Psaumes 88.8 Psaumes 38.11 Psaumes 31.11 Job 19.12-19.15

Cette Bible est dans le domaine public.