Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 84.3
Bible en Swahili de l’est


1 Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi!Psaumes 27.4 Psaumes 43.3 Psaumes 132.5 Psaumes 36.8 Psaumes 8.1
2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.Psaumes 42.1-42.2 Psaumes 73.26 Psaumes 143.6 Psaumes 119.81 Esaïe 26.9
3 Shomoro naye ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kioto, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee Bwana wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu.Psaumes 5.2 Psaumes 90.1 Matthieu 23.37 Psaumes 116.7 Psaumes 91.1
4 Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.Psaumes 65.4 Psaumes 27.4 Psaumes 42.5 Psaumes 71.8 Psaumes 145.1-145.2
5 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.Psaumes 40.8 Michée 4.2 Jérémie 50.4-50.5 Esaïe 45.24 Psaumes 81.1
6 Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika barakaPsaumes 68.9 Romains 5.3-5.5 Joël 2.23 Apocalypse 7.14 2 Samuel 5.22-5.24
7 Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.2 Corinthiens 3.18 Proverbes 4.18 Esaïe 40.31 Deutéronome 16.16 2 Pierre 3.18
8 Bwana, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize,Psaumes 59.5
9 Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi wako.Psaumes 2.2 Genèse 15.1 Psaumes 89.20 2 Chroniques 6.42 Psaumes 59.11
10 Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu.Psaumes 27.4 Psaumes 63.2 Psaumes 26.8-26.10 Psaumes 141.4-141.5 Philippiens 3.20
11 Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.Proverbes 2.7 Psaumes 34.9-34.10 Matthieu 6.33 Psaumes 85.12 Philippiens 4.19
12 Ee Bwana wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.Psaumes 62.8 Psaumes 2.12 Esaïe 50.10 Esaïe 30.18 Psaumes 34.8

Cette Bible est dans le domaine public.