Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 54
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. 2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu. 3 Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao. 4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu. 5 Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. 6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema. 7 Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.

Cette Bible est dans le domaine public.