1  Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. 
Psaumes 14.1-14.7  Psaumes 10.4  Romains 3.10-3.31  Psaumes 88.1  1 Rois 14.24  
 2  Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. 
2 Chroniques 15.2  Psaumes 27.8  2 Chroniques 19.3  Psaumes 111.10  Esaïe 55.6  
 3  Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. 
Romains 3.12  Esaïe 64.6  Esaïe 53.6  Jérémie 8.5-8.6  Psaumes 14.3  
 4  Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU. 
Jérémie 4.22  Psaumes 94.8  Esaïe 27.11  Matthieu 23.17-23.39  Apocalypse 17.16  
 5  Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau. 
Lévitique 26.17  Proverbes 28.1  Lévitique 26.36  Ezéchiel 6.5  Psaumes 141.7  
 6  Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi. 
Psaumes 14.7  Esaïe 14.32  Esdras 3.11  Néhémie 12.43  Jérémie 30.18