Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 47.7
Bible en Swahili de l’est


1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. 2 Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. 3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. 4 Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda. 5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu. 6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni. 7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili. 8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. 9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.

Cette Bible est dans le domaine public.