Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 24.10
Bible en Swahili de l’est


1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.Psaumes 89.11 1 Corinthiens 10.26 Exode 9.29 Job 41.11 1 Chroniques 29.11
2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.Psaumes 136.6 Genèse 1.9-1.10 Psaumes 104.5-104.6 Jérémie 5.22 Psaumes 96.10
3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?Psaumes 15.1 Psaumes 2.6 Malachie 3.1 Psaumes 68.18 Hébreux 12.28
4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.Matthieu 5.8 Psaumes 51.10 Job 17.9 Jacques 4.8 Psaumes 26.6
5 Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.Tite 3.4-3.6 Psaumes 88.1 Philippiens 3.9 Esaïe 46.13 Esaïe 61.10
6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.Psaumes 27.8 Psaumes 105.4 1 Pierre 2.9 Jean 1.47 Psaumes 22.30
7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.1 Corinthiens 2.8 Esaïe 26.2 Psaumes 118.19-118.20 Psaumes 97.6 Psaumes 132.8
8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.Apocalypse 6.2 Apocalypse 19.11-19.21 Exode 15.3 Esaïe 63.1-63.6 Psaumes 93.1
9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. 10 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.Tite 2.13 Matthieu 25.31 Esaïe 6.3-6.5 Matthieu 25.34 Jean 14.9

Cette Bible est dans le domaine public.