Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 138.6
Bible en Swahili de l’est


1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi. 2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote. 3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu. 4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako. 5 Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu. 6 Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali. 7 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa. 8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

Cette Bible est dans le domaine public.