Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 114.1
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. 2 Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. 3 Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. 4 Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. 5 Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma? 6 Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo? 7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo. 8 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.

Cette Bible est dans le domaine public.