Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 113.4
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana. 2 Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele. 3 Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa. 4 Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu. 5 Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu; 6 Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani? 7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. 8 Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake. 9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Cette Bible est dans le domaine public.