Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 5.20
Bible en Swahili de l’est


1 Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?Job 15.15 Job 15.8-15.10 Ephésiens 1.1 Esaïe 41.21-41.23 Esaïe 41.1
2 Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.Romains 2.8 1 Samuel 18.8-18.9 Ecclésiaste 7.9 Psaumes 14.1 Genèse 30.1
3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara niliyalaani maskani yake.Psaumes 73.18-73.20 Psaumes 37.35-37.36 Job 27.8 Psaumes 69.25 Job 24.18
4 Watoto wake wako mbali na wokovu, Nao wamesongwa langoni, Wala hapana atakayewaponya.Psaumes 127.5 Psaumes 119.155 Job 8.4 Job 18.16-18.19 Job 4.10-4.11
5 Mavuno yake wale wenye njaa huyala, Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani, Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.Job 1.17 Jérémie 51.34 Job 2.3 Job 1.15 Job 20.15
6 Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi;Psaumes 90.7 Esaïe 45.7 Job 34.29 Hébreux 12.15 1 Samuel 6.9
7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka, Kama cheche za moto zirukavyo juu.Job 14.1 Genèse 3.17-3.19 1 Corinthiens 10.13 Ecclésiaste 1.8 Psaumes 90.8-90.9
8 Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu;Psaumes 50.15 Psaumes 37.5 1 Pierre 4.19 Genèse 32.7-32.12 Job 8.5
9 Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;Psaumes 40.5 Job 9.10 Psaumes 72.18 Romains 11.33 Job 37.5
10 Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani;Psaumes 147.8 Jérémie 5.24 Jérémie 14.22 Actes 14.17 Psaumes 65.9-65.11
11 Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama.1 Samuel 2.7-2.8 Luc 1.52-1.53 Psaumes 113.7 Ezéchiel 17.24 Jacques 4.6-4.10
12 Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.Néhémie 4.15 Esaïe 8.10 Psaumes 33.10-33.11 Psaumes 21.11 Proverbes 21.30
13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.Luc 1.51 1 Corinthiens 3.19 Psaumes 9.15-9.16 1 Corinthiens 1.19-1.20 Psaumes 35.7-35.8
14 Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku.Job 12.25 Deutéronome 28.29 Esaïe 59.10 Proverbes 4.19 Amos 8.9
15 Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.Psaumes 35.10 Psaumes 10.17 Psaumes 107.41 Psaumes 10.14 Psaumes 109.31
16 Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake.Psaumes 107.42 1 Samuel 2.8-2.9 Psaumes 63.11 Psaumes 9.18 Exode 11.7
17 Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.Psaumes 94.12 Hébreux 12.5-12.11 Jacques 1.12 Jérémie 31.18 Apocalypse 3.19
18 Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.Osée 6.1 Deutéronome 32.39 1 Samuel 2.6 Esaïe 30.26 Psaumes 147.3
19 Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.Psaumes 34.19 1 Corinthiens 10.13 Proverbes 24.16 2 Pierre 2.9 Psaumes 91.3-91.10
20 Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.Psaumes 33.19 Psaumes 37.19 Proverbes 10.3 Esaïe 33.16 Habakuk 3.17
21 Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.Psaumes 31.20 Jacques 3.5-3.8 Proverbes 12.18 Psaumes 57.4 Psaumes 91.5-91.7
22 Wewe utayacheka maangamizo na njaa; Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.Ezéchiel 34.25 Esaïe 35.9 Esaïe 65.25 Psaumes 91.13 2 Rois 19.21
23 Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara; Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.Psaumes 91.12-91.13 Lévitique 26.6 Ezéchiel 14.15-14.16 Romains 8.38-8.39 Daniel 6.22
24 Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama; Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.Job 18.6 Psaumes 91.10 Psaumes 121.7-121.8 1 Samuel 30.3 Psaumes 25.13
25 Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.Psaumes 112.2 Psaumes 72.16 Esaïe 44.3-44.4 Deutéronome 28.4 Psaumes 127.3-127.5
26 Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.Genèse 15.15 Proverbes 9.11 Proverbes 10.27 Genèse 25.8 Job 42.16-42.17
27 Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo; Yasikie, uyajue, ili upate mema.Psaumes 111.2 Proverbes 9.12 Job 22.2 Job 32.11-32.12 Job 8.8-8.10

Cette Bible est dans le domaine public.