Juda à partir du schisme
Division du royaume
 1  Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme. 
Genèse 12.6  1 Rois 12.1-12.20  Genèse 37.12-37.13  1 Rois 4.1  1 Chroniques 12.38  
 2  Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri. 
1 Rois 11.40  1 Rois 12.2  1 Rois 11.28  1 Rois 11.26  
 3  Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 
1 Rois 12.3  
 4  Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 
Exode 2.23  1 Jean 5.3  1 Rois 9.22  1 Rois 12.4  Matthieu 23.4  
 5  Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao. 
Proverbes 3.28  1 Rois 12.5  
 6  Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa? 
Job 32.7  Jérémie 42.20  Job 12.12-12.13  Proverbes 27.10  Proverbes 12.15  
 7  Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote. 
Proverbes 15.1  1 Rois 12.7  Genèse 49.21  2 Samuel 15.2-15.6  
 8  Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake. 
2 Samuel 17.14  Proverbes 13.20  Proverbes 19.20  Proverbes 1.25  Esaïe 30.1  
 9  Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako. 
2 Samuel 17.5-17.6  2 Chroniques 10.6  1 Rois 22.6-22.8  
 10  Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 
Esaïe 19.11-19.13  1 Rois 12.10-12.11  Proverbes 14.16  Proverbes 29.23  2 Samuel 17.7-17.13  
 11  Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. 
Apocalypse 9.10  Exode 5.18  1 Samuel 8.18  Esaïe 47.6  Jérémie 28.13-28.14  
 12  Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 
1 Rois 12.12-12.15  2 Chroniques 10.5  
 13  Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana, 
Genèse 42.30  Proverbes 15.1  1 Samuel 25.10-25.11  2 Chroniques 10.8  1 Rois 20.6-20.11  
 14  akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. 
Ecclésiaste 7.8  Daniel 6.7  2 Chroniques 22.4-22.5  Ecclésiaste 10.16  Jacques 3.14-4.2  
 15  Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni. 
2 Chroniques 25.16-25.20  1 Samuel 2.25  1 Rois 11.29-11.39  Esaïe 19.14  Actes 2.23  
 16  Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao. 
2 Samuel 20.1  2 Chroniques 10.19  Juges 8.35  1 Samuel 22.9  1 Rois 12.16-12.17  
 17  Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao. 
1 Rois 12.17  2 Chroniques 11.1  1 Rois 11.36  
 18  Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu. 
1 Rois 5.14  1 Rois 4.6  Actes 7.57-7.58  2 Chroniques 24.21  
 19  Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo. 
2 Chroniques 5.9  Esdras 9.7  2 Rois 17.21-17.23  Psaumes 89.30  Josué 4.9