Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 24.10 Bible en Swahili de l’est
1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. 3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? 4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. 5 Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. 6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. 7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. 8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita. 9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.10 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.