Adresse et salutation
 1  Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; 
Romains 1.1  1 Timothée 6.3  Tite 2.11-2.12  2 Timothée 2.23  2 Pierre 1.3  
 2  katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; 
2 Timothée 1.1  Tite 3.7  2 Timothée 1.9  Tite 2.13  Hébreux 6.17-6.18  
 3  akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu; 
1 Timothée 1.11  1 Timothée 1.1  Tite 2.10  Tite 3.4-3.6  Apocalypse 14.16  
 4  kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu. 
Jude 1.3  2 Timothée 1.2  2 Pierre 1.1  2 Corinthiens 2.13  Galates 2.3  
Mission de Tite
 5  Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; 
Actes 14.23  1 Timothée 1.3  Actes 27.7  2 Timothée 2.2  Ecclésiaste 12.9  
 6  ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. 
1 Timothée 3.12  1 Timothée 3.2-3.7  Tite 1.6-1.8  Ezéchiel 44.22  Tite 1.10  
 7  Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu. 
2 Pierre 2.10  1 Pierre 5.2  Luc 12.42  Ephésiens 5.18  Lévitique 10.9  
 8  bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; 
1 Timothée 3.2  1 Thessaloniciens 2.10  2 Timothée 3.3  1 Timothée 6.11  2 Corinthiens 6.4-6.8  
 9  akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga. 
1 Timothée 1.10  2 Thessaloniciens 2.15  1 Timothée 6.3  2 Timothée 1.13  Tite 2.1  
 10  Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. 
1 Timothée 1.6  Actes 11.2  Apocalypse 2.6  1 Jean 2.18  2 Timothée 4.4  
 11  Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. 
2 Timothée 3.6  1 Timothée 6.5  Esaïe 56.10-56.11  Jérémie 8.10  Psaumes 63.11  
 12  Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu. 
Actes 17.28  1 Timothée 4.2  Actes 2.11  Romains 16.18  2 Pierre 2.15  
 13  Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani; 
Tite 2.2  2 Corinthiens 13.10  Tite 2.15  1 Timothée 5.20  2 Timothée 4.2  
 14  wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli. 
Colossiens 2.22  2 Timothée 4.4  Hébreux 12.25  Matthieu 15.9  2 Pierre 2.22  
 15  Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia. 
Romains 14.20  Romains 14.14  Romains 14.23  1 Corinthiens 10.23  1 Timothée 4.3-4.4  
 16  Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. 
1 Jean 2.4  Esaïe 29.13  Ezéchiel 33.31  2 Timothée 3.5-3.8  Jude 1.4