Devoirs envers les autorités
 1  Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 
Tite 3.1  Jean 19.11  1 Pierre 2.13-2.17  Jude 1.8  Ephésiens 5.21  
 2  Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 
Tite 3.1  1 Pierre 2.13  Esaïe 58.2  Matthieu 23.13  Jérémie 44.14-44.17  
 3  Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 
1 Pierre 3.13-3.14  Ecclésiaste 10.4-10.6  Romains 13.4  Proverbes 14.35  Jérémie 22.15-22.18  
 4  kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 
Romains 12.19  2 Chroniques 19.6  Proverbes 24.23-24.24  1 Thessaloniciens 4.6  Proverbes 20.2  
 5  Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 
1 Pierre 2.19  Ecclésiaste 8.2  1 Pierre 3.16  Actes 24.16  Hébreux 13.18  
 6  Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 
Matthieu 22.17-22.21  Matthieu 17.24-17.27  Marc 12.14-12.17  Luc 20.21-20.26  Exode 18.13-18.27  
 7  Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. 
Matthieu 17.25  Luc 20.25  1 Timothée 5.17  Matthieu 22.21  1 Samuel 12.18  
Devoirs envers les autres
 8  Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. 
Romains 13.10  Matthieu 7.12  Galates 5.14  Matthieu 22.39-22.40  Jacques 2.8  
 9  Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 
Lévitique 19.18  Matthieu 19.18-19.19  Exode 20.12-20.17  Romains 7.7-7.8  Luc 10.27  
 10  Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. 
Romains 13.8  Matthieu 22.39-22.40  1 Corinthiens 13.4-13.7  
 11  Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 
Ephésiens 5.14  1 Corinthiens 15.34  Luc 21.28  1 Pierre 4.7  1 Thessaloniciens 5.5-5.8  
 12  Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 
Ephésiens 5.11  2 Corinthiens 6.7  Esaïe 30.22  Esaïe 2.20  Ezéchiel 18.31-18.32  
 13  Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 
Galates 5.21  1 Thessaloniciens 4.3-4.5  1 Thessaloniciens 4.12  Luc 21.34  Ephésiens 5.18  
 14  Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. 
Galates 3.27  Ephésiens 4.24  Galates 5.24  1 Pierre 2.11  Romains 8.12-8.13