Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Habakuk 3
Bible en Swahili de l’est


1 Sala ya nabii Habakuki. Psaumes 86.1-86.17 Psaumes 90.1-90.17 Psaumes 7.1-7.17
2 Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Psaumes 85.6 Psaumes 119.120 Habakuk 3.16 Osée 6.2-6.3 Lamentations 3.32
3 Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake. Deutéronome 33.2 Amos 1.12 Abdias 1.9 Esaïe 6.3 Genèse 21.21
4 Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake. Job 26.14 Exode 14.20 Esaïe 60.19-60.20 Psaumes 104.2 Exode 13.21
5 Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake. Exode 12.29-12.30 Nombres 16.46-16.49 Psaumes 18.7-18.13 Nombres 14.12 Deutéronome 32.24
6 Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale. Genèse 49.26 Nahum 1.5 Deutéronome 33.15 Psaumes 68.16 Luc 1.50
7 Naliziona hema za Kushani katika taabu; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka. Exode 15.14-15.16 Genèse 25.1-25.4 Nombres 22.3-22.4 Psaumes 83.5-83.10 Josué 2.10
8 Je! Bwana aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi zako, Katika magari yako ya wokovu? Psaumes 68.17 Psaumes 114.5 Psaumes 18.10 Esaïe 50.2 Esaïe 19.1
9 Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito. Psaumes 7.12-7.13 Psaumes 105.41 Psaumes 78.15-78.16 Hébreux 6.13-6.18 Esaïe 51.9-51.10
10 Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake. Psaumes 93.3 Hébreux 11.29 Psaumes 98.7-98.8 Psaumes 97.4-97.5 Exode 19.16-19.18
11 Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao. Psaumes 18.12-18.14 Psaumes 144.5-144.6 Psaumes 77.17-77.18 Esaïe 38.8 Josué 10.11-10.13
12 Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira. Michée 4.12-4.13 Jérémie 51.33 Psaumes 44.1-44.3 Actes 13.19 Josué 6.1-6.12
13 Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani. Psaumes 110.6 Psaumes 105.15 Psaumes 105.26 Josué 10.11 Esaïe 63.11
14 Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri. Psaumes 10.8 Daniel 11.40 Zacharie 9.14 Exode 1.10-1.16 Juges 7.22
15 Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako, Chungu ya maji yenye nguvu. Psaumes 77.19 Habakuk 3.8 Exode 15.8
16 Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu. Daniel 10.8 Habakuk 3.2 Jérémie 23.9 Jérémie 15.10-15.11 Habakuk 1.5-1.11
17 Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; Deutéronome 28.15-28.18 Amos 4.6-4.10 Joël 1.16-1.18 Jérémie 5.17 Joël 1.10-1.13
18 Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. Job 13.15 Esaïe 61.10 Psaumes 46.1-46.5 Psaumes 25.5 Philippiens 4.4
19 YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka. Psaumes 18.33 2 Samuel 22.34 Deutéronome 33.29 Deutéronome 32.13 2 Corinthiens 12.9-12.10

Cette Bible est dans le domaine public.