Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Habakuk 1.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo aliouona nabii Habakuki.Nahum 1.1 Esaïe 22.1
2 Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.Jérémie 14.9 Lamentations 3.8 Psaumes 13.1-13.2 Psaumes 22.1-22.2 Psaumes 94.3
3 Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.Psaumes 55.9-55.11 Matthieu 10.16 Psaumes 73.3-73.9 Michée 7.1-7.4 Jérémie 20.8
4 Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.Psaumes 119.126 Ezéchiel 9.9 Job 21.7 Esaïe 1.21-1.23 Jérémie 12.1
5 Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.Esaïe 29.14 Ezéchiel 12.22-12.28 Jérémie 9.25-9.26 Jérémie 18.18 Deutéronome 4.27
6 Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.2 Rois 24.2 Jérémie 5.15 Jérémie 21.4 Jérémie 25.9 Jérémie 4.8
7 Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.Jérémie 39.5-39.9 Jérémie 52.9-52.11 Jérémie 52.25-52.27 Esaïe 18.7 Deutéronome 5.27
8 Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.Jérémie 4.13 Sophonie 3.3 Jérémie 5.6 Osée 8.1 Ezéchiel 17.3
9 Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.Osée 13.15 Habakuk 1.6 Habakuk 2.5-2.13 Genèse 41.49 Jérémie 25.9
10 Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa.2 Chroniques 36.6 Jérémie 32.24 2 Chroniques 36.10 Esaïe 14.16 Jérémie 52.4-52.7
11 Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.Jérémie 4.11-4.12 Daniel 5.20 Daniel 4.30-4.34 Daniel 5.3-5.4
12 Ee Bwana, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee Bwana, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.Deutéronome 32.4 Jérémie 30.11 Jérémie 46.28 Psaumes 90.2 Deutéronome 33.27
13 Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;Psaumes 34.15-34.16 Psaumes 10.15 Psaumes 50.21 Jérémie 12.1-12.2 Actes 3.13-3.15
14 na kufanya wanadamu kuwa kama samaki wa baharini, kama vitu vitambaavyo, ambavyo havina mtawala?Proverbes 6.7
15 Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika juya lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.Jérémie 16.16 Amos 4.2 Psaumes 10.9 Ezéchiel 25.6 Ezéchiel 35.15
16 Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka, na kulifukizia uvumba juya lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele.Habakuk 1.11 Esaïe 37.24 Daniel 4.30 Esaïe 10.13-10.15 Deutéronome 8.17
17 Je! Atawatoa walio katika wavu wake, asiache kuwaua watu wa mataifa daima?Esaïe 14.6 Habakuk 1.9-1.10 Jérémie 46.1-46.28 Habakuk 2.17 Esaïe 19.8

Cette Bible est dans le domaine public.