Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 1.12
Bible en Swahili de l’est


1 Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!Esaïe 3.26 1 Rois 4.21 Esdras 4.20 Apocalypse 18.16-18.17 Lamentations 5.16
2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake.Psaumes 6.6 Michée 7.5 Jérémie 9.1 Jérémie 13.17 Lamentations 1.16-1.17
3 Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya makafiri, Haoni raha iwayo yote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake.Deutéronome 28.64-28.67 Lamentations 2.9 Jérémie 52.27-52.30 Lévitique 26.36-26.39 2 Chroniques 36.20-36.21
4 Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.Joël 1.8-1.13 Jérémie 9.11 Jérémie 10.22 Jérémie 14.2 Lamentations 2.6-2.7
5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.Jérémie 30.14-30.15 Psaumes 90.7-90.8 Jérémie 39.9 Ezéchiel 8.17-8.18 Ezéchiel 9.9
6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.Ezéchiel 24.25 Ezéchiel 7.20-7.22 Lamentations 2.1-2.7 Josué 7.12-7.13 Ezéchiel 11.22-11.23
7 Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.Psaumes 42.4 Psaumes 77.5-77.9 Psaumes 79.4 Psaumes 77.3 Job 29.2-30.1
8 Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.Esaïe 59.2-59.13 Lamentations 1.20-1.22 Lamentations 1.11 Lamentations 1.4-1.5 Jérémie 13.22
9 Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, Bwana, teso langu; Maana huyo adui amejitukuza.Deutéronome 32.29 Esaïe 47.7 Ecclésiaste 4.1 Lamentations 1.17 Psaumes 25.18
10 Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamaniko yake yote; Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.Jérémie 51.51 Deutéronome 23.3 Lamentations 1.7 Esaïe 64.10-64.11 Néhémie 13.1
11 Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee Bwana, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.Jérémie 52.6 Jérémie 38.9 Lamentations 2.12 Lamentations 2.20 Ezéchiel 4.15-4.17
12 Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo Bwana amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.Luc 23.28-23.31 Daniel 9.12 Lamentations 2.13 Matthieu 24.21 Esaïe 13.13
13 Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu, Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu, Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.Habakuk 3.16 Job 30.30 Ezéchiel 17.20 Job 19.6 Psaumes 22.14
14 Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;Deutéronome 28.48 Esaïe 47.6 Ezéchiel 25.4 Proverbes 5.22 Jérémie 28.14
15 Bwana amenitia mikononi mwao, Ambao siwezi kupingamana nao. Bwana amewafanya mashujaa wangu wote Kuwa si kitu kati yangu; Ameita mkutano mkuu kinyume changu Ili kuwaponda vijana wangu; Bwana amemkanyaga kama shinikizoni Huyo bikira binti Yuda.Malachie 4.3 Esaïe 28.18 Esaïe 63.3 Juges 10.8 Esaïe 5.5
16 Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; Kwa kuwa mfariji yu mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.Lamentations 1.2 Lamentations 3.48-3.49 Jérémie 14.17 Lamentations 2.11 Lamentations 2.18
17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.Jérémie 4.31 Esaïe 1.15 Lamentations 1.9 2 Rois 24.2-24.4 Lamentations 1.16
18 Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.Jérémie 12.1 1 Samuel 12.14-12.15 Lamentations 1.12 Psaumes 119.75 1 Rois 13.21
19 Naliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao.Lamentations 1.2 Lamentations 2.20 Lamentations 1.11 Job 19.13-19.19 Lamentations 5.12
20 Angalia, Ee Bwana; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti.Lamentations 2.11 Ezéchiel 7.15 Deutéronome 32.25 Esaïe 16.11 Job 30.27
21 Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.Lamentations 1.8 Lamentations 1.22 Lamentations 1.16 Jérémie 50.11 Lamentations 2.15
22 Huo uovu wao wote Na uje mbele zako wewe; Ukawatende wao kama ulivyonitenda mimi Kwa dhambi zangu zote; Kwa maana mauguzi yangu ni mengi sana, Na moyo wangu umezimia.Néhémie 4.4-4.5 Jérémie 8.18 Psaumes 109.14-109.15 Ephésiens 3.13 Psaumes 137.7-137.9

Cette Bible est dans le domaine public.