Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Cantique 7.3
Bible en Swahili de l’est


1 Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika mitalawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi;Psaumes 45.13 Luc 15.22 Daniel 2.32 Exode 35.35 Colossiens 2.19
2 Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;Esaïe 46.3 Proverbes 3.8 Cantique 5.14 Jérémie 1.5 Romains 7.4
3 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Ambao ni mapacha ya paa;Cantique 4.5 Cantique 6.6
4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski;Cantique 4.4 Psaumes 144.12 Cantique 6.5 2 Samuel 8.6 Philippiens 1.9-1.10
5 Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungu yake.Esaïe 35.2 Cantique 4.1 Genèse 32.26 Colossiens 1.18 Apocalypse 1.14
6 Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa!Cantique 1.15-1.16 Cantique 4.10 Psaumes 45.11 Sophonie 3.17 Cantique 2.14
7 Kimo chako kimefanana na mtende, Na maziwa yako na vichala.Cantique 4.5 Ephésiens 4.13 Cantique 8.8 Psaumes 92.12 Cantique 7.8
8 Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera;2 Corinthiens 2.14 Cantique 1.3 Jérémie 32.41 Cantique 2.5 Cantique 4.16-5.1
9 Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao.Cantique 5.16 Esaïe 62.8-62.9 Cantique 5.2 Cantique 2.14 Actes 2.11-2.13
10 Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.Cantique 2.16 Psaumes 45.11 Cantique 6.3 Galates 2.20 Psaumes 147.11
11 Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji.Cantique 4.8 Cantique 1.4 Cantique 2.10-2.13
12 Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.Cantique 6.11 Ephésiens 6.24 Psaumes 43.4 Cantique 2.15 Psaumes 73.25
13 Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu.Genèse 30.14 Matthieu 13.52 Philippiens 1.11 1 Corinthiens 16.2 1 Pierre 4.11

Cette Bible est dans le domaine public.