Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 99.6
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.Psaumes 97.1 Exode 25.22 Psaumes 80.1 Esaïe 24.19-24.20 Psaumes 93.1
2 Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote.Psaumes 97.9 Psaumes 113.4 Esaïe 12.6 Daniel 4.34-4.35 Psaumes 76.1-76.2
3 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu.Esaïe 6.3 Josué 24.19 Deutéronome 28.58 1 Samuel 2.2 Psaumes 111.9
4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.Psaumes 11.7 Jérémie 23.5 Esaïe 42.4 Psaumes 72.1-72.2 Job 37.23
5 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu.Psaumes 132.7 Psaumes 34.3 Esaïe 25.1 Psaumes 99.3 Exode 15.2
6 Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia;Jérémie 15.1 Exode 24.6-24.8 Exode 15.25 Exode 14.15 Nombres 16.21-16.22
7 Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.Exode 33.9 Nombres 12.5 1 Samuel 12.3-12.5 Deutéronome 4.5 1 Jean 3.21-3.22
8 Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.Jérémie 46.28 Nombres 20.12 Psaumes 89.33 Nombres 14.20-14.34 Nombres 20.24
9 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.Apocalypse 4.8 Esaïe 57.15 Psaumes 99.5 Psaumes 99.3 Psaumes 2.6

Cette Bible est dans le domaine public.