Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 79.10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.2 Chroniques 36.19 Jérémie 26.18 Michée 3.12 Lamentations 1.10 Jérémie 52.13
2 Wameziacha maiti za watumishi wako Ziwe chakula cha ndege wa angani. Na miili ya watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi.Jérémie 7.33 Jérémie 34.20 Jérémie 16.4 Deutéronome 28.26 Jérémie 15.3
3 Wamemwaga damu yao kama maji Pande zote za Yerusalemu, Wala hapakuwa na mzishi.Jérémie 16.4 Jérémie 14.16 Apocalypse 18.24 Apocalypse 17.6 Jérémie 25.33
4 Tumekuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.Psaumes 80.6 Jérémie 24.9 Lamentations 2.15-2.16 Psaumes 89.41 Ezéchiel 36.15
5 Ee Bwana, hata lini? Utaona hasira milele? Wivu wako utawaka kama moto?Psaumes 89.46 Psaumes 85.5 Psaumes 74.1 Deutéronome 29.20 Sophonie 3.8
6 Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua, Na falme za hao wasioliitia jina lako.Jérémie 10.25 2 Thessaloniciens 1.8 Psaumes 14.4 Psaumes 69.24 Psaumes 53.4
7 Kwa maana wamemla Yakobo, Na matuo yake wameyaharibu.2 Chroniques 36.21 Esaïe 24.1-24.12 Psaumes 80.13 Zacharie 1.15 Jérémie 51.34-51.35
8 Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu, Rehema zako zije kutulaki hima, Kwa maana tumedhilika sana.Psaumes 116.6 Psaumes 142.6 Esaïe 64.9 Psaumes 21.3 Deutéronome 28.43
9 Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, utughofiri dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako.Jérémie 14.7 2 Chroniques 14.11 Psaumes 25.11 Psaumes 65.3 Jérémie 14.21
10 Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulike kati ya mataifa machoni petu.Psaumes 42.10 Psaumes 42.3 Psaumes 94.1 Psaumes 115.2 Psaumes 9.16
11 Kuugua kwake aliyefungwa Na kuingie mbele zako. Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako Uwahifadhi wana wa mauti.Psaumes 102.20 Esaïe 33.2 Ephésiens 3.20 Exode 2.23-2.24 Psaumes 69.33
12 Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.Genèse 4.15 Jérémie 32.18 Lévitique 26.28 Lévitique 26.21 Luc 6.38
13 Na sisi tulio watu wako, Na kondoo za malisho yako, Tutakushukuru milele; Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.Psaumes 74.1 Psaumes 95.7 Esaïe 43.21 Psaumes 100.3 Psaumes 145.4

Cette Bible est dans le domaine public.