1  Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu. 
Psaumes 145.18  Psaumes 138.2  Psaumes 76.1  Psaumes 57.1  Psaumes 44.1  
 2  Nitakapoufikia wakati ulioamriwa, Mimi nitahukumu hukumu za haki. 
Actes 17.31  Psaumes 101.2  2 Samuel 5.3  Jean 7.6  2 Samuel 8.15  
 3  Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki, Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake. 
1 Samuel 2.8  Esaïe 24.19  Psaumes 78.60-78.72  2 Samuel 5.2  Hébreux 1.3  
 4  Naliwaambia waliojivuna, Msijivune; Na wasio haki, Msiiinue pembe. 
Zacharie 1.21  Psaumes 148.14  Proverbes 9.6  Psaumes 89.17  Proverbes 8.5  
 5  Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi. 
Exode 32.9  Actes 7.51  2 Chroniques 30.8  Deutéronome 31.27  Esaïe 48.4  
 6  Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima. 
Psaumes 3.3  
 7  Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu. 
Psaumes 50.6  Daniel 2.21-2.22  1 Samuel 15.23  1 Samuel 2.7-2.8  2 Samuel 3.17-3.18  
 8  Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa. 
Job 21.20  Psaumes 11.6  Proverbes 23.30  Jérémie 25.15  Apocalypse 14.9-14.10  
 9  Bali mimi nitatangaza matendo yako milele, Nitamwimbia Mungu wa Yakobo. 
Psaumes 104.33  Psaumes 40.10  Psaumes 9.14  Psaumes 145.1-145.2  
 10  Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka. 
Psaumes 89.17  Psaumes 92.10  Jérémie 48.25  Psaumes 148.14  Psaumes 101.8