Prière pour la délivrance
 1  Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.  
2  Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.  
3  Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!  
4  Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.  
5  Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.