Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 15
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Psaumes 61.4 Psaumes 92.13 Psaumes 84.4 Psaumes 24.3-24.5 Psaumes 2.6
2 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Ephésiens 4.25 Colossiens 3.9 Proverbes 28.18 Psaumes 34.12-34.13 Luc 1.6
3 Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake. Romains 13.10 Psaumes 101.5-101.8 Lévitique 19.16 3 Jean 1.11 Matthieu 7.12
4 Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. Matthieu 5.33 Juges 11.35 Psaumes 101.6 Jacques 2.1-2.9 Job 32.21-32.22
5 Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele. Exode 22.25 Ezéchiel 22.12 Deutéronome 16.19 Ezéchiel 18.8 Deutéronome 23.19-23.20

Cette Bible est dans le domaine public.