Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 141.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.Psaumes 70.5 Psaumes 40.13 Job 7.21 Psaumes 143.1 Psaumes 22.19
2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.Apocalypse 8.3-8.4 1 Timothée 2.8 Apocalypse 5.8 Exode 29.39 Psaumes 134.2
3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.Michée 7.5 Jacques 1.26 Psaumes 39.1 Jacques 3.2 Psaumes 17.3-17.5
4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.1 Corinthiens 15.33 Esaïe 63.17 1 Rois 8.58 2 Corinthiens 6.17 Psaumes 119.36
5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.Proverbes 19.25 Proverbes 25.12 Galates 6.1 2 Timothée 1.16-1.18 Proverbes 9.8-9.9
6 Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.2 Samuel 1.17-1.27 1 Chroniques 10.1-10.7 2 Samuel 5.1-5.3 2 Samuel 2.4-2.6 1 Samuel 31.1-31.8
7 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.Psaumes 53.5 Hébreux 11.37 2 Corinthiens 1.9 1 Samuel 22.18-22.19 Romains 8.36
8 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.Psaumes 25.15-25.17 Psaumes 123.1-123.2 Psaumes 102.17 Esaïe 41.17 2 Chroniques 20.12
9 Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.Psaumes 140.5 Psaumes 119.110 Psaumes 38.12 Proverbes 13.14 Psaumes 142.3
10 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.Psaumes 35.8 Proverbes 11.8 Esther 7.10 Psaumes 140.9 Psaumes 64.7-64.8

Cette Bible est dans le domaine public.