Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 128.4
Bible en Swahili de l’est


1 Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. 2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. 3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. 4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. 5 Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; 6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Cette Bible est dans le domaine public.