Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 127.5
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. 2 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi. 3 Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. 4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani. 5 Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.

Cette Bible est dans le domaine public.