Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 52.1
Bible en Swahili de l’est


1 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. 2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila 3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. 4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. 5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai. 6 Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; 7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake. 8 Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. 9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

Cette Bible est dans le domaine public.