Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 13
Bible en Swahili de l’est


1 Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi. Psaumes 51.2 Ezéchiel 36.25 Jean 1.29 1 Corinthiens 6.11 1 Jean 5.6
2 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi. Osée 2.17 Jérémie 23.14-23.15 Ezéchiel 36.25 1 Rois 22.22 Ezéchiel 30.13
3 Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii. Deutéronome 13.6-13.11 Deutéronome 18.20 Matthieu 10.37 Exode 32.27-32.28 Jérémie 23.34
4 Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii, kila mmoja wao, atayaonea haya maono yake atoapo unabii; wala hawatavaa joho ya nywele ili kudanganya watu; 2 Rois 1.8 Matthieu 3.4 Esaïe 20.2 Michée 3.6-3.7 Marc 1.6
5 bali atasema, Mimi si nabii kamwe; mimi ni mkulima wa nchi; kwa maana nalifanywa mtumwa tokea ujana wangu. Amos 7.14 Actes 19.17-19.20
6 Na mtu atamwambia, Je! Jeraha hizi ulizo nazo kati ya mikono yako ni nini? Naye atajibu, Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu. Proverbes 27.5-27.6 1 Rois 18.28 Psaumes 22.16 Jean 19.14-19.16 Jean 18.35
7 Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema Bwana wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo. Marc 14.27 Esaïe 40.11 Matthieu 26.31 Zacharie 11.7 Jérémie 23.5-23.6
8 Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo. Ezéchiel 5.12 Ezéchiel 5.2-5.4 Esaïe 6.13 1 Thessaloniciens 2.15-2.16 Esaïe 66.24
9 Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu. Esaïe 48.10 Psaumes 50.15 1 Pierre 1.6-1.7 Jérémie 29.11-29.12 Zacharie 10.6

Cette Bible est dans le domaine public.