Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 10.6
Bible en Swahili de l’est


1 Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.Jérémie 10.13 Ezéchiel 34.26 Esaïe 44.3 Jérémie 14.22 Jacques 5.7
2 Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.Ezéchiel 34.5 Matthieu 9.36 Osée 3.4 Genèse 31.19 Habakuk 2.18
3 Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.Ezéchiel 34.16-34.17 Sophonie 2.7 Ruth 1.6 Jérémie 25.12 Sophonie 1.8
4 Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila mtawala pamoja.Zacharie 9.10 Nombres 24.17 Zacharie 9.8 Zacharie 1.20-1.21 Ephésiens 4.8-4.11
5 Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.Aggée 2.22 Psaumes 20.7 Romains 8.31-8.37 Michée 7.10 Actes 18.24
6 Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia.Zacharie 13.9 Zacharie 10.12 Jérémie 3.18 Esaïe 14.1 Jérémie 31.31
7 Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana.Zacharie 9.15 Proverbes 31.6-31.7 Psaumes 90.16 Psaumes 28.7 Psaumes 104.15
8 Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka.Esaïe 5.26 Jérémie 33.22 Esaïe 7.18 Ezéchiel 36.10-36.11 Jérémie 31.10-31.11
9 Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi.Ezéchiel 6.9 1 Rois 8.47-8.48 Osée 2.23 Jérémie 31.27 Actes 8.4
10 Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana.Osée 11.11 Michée 7.14 Esaïe 11.11-11.16 Esaïe 27.12-27.13 Esaïe 54.2-54.3
11 Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.Ezéchiel 30.13 Michée 5.5-5.6 Esaïe 14.25 Psaumes 114.3 Esaïe 43.2
12 Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina lake, asema Bwana.Michée 4.5 Zacharie 10.6 Genèse 24.40 Esaïe 45.24 Genèse 5.24

Cette Bible est dans le domaine public.