Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 10.1
Bible en Swahili de l’est


1 Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.Jérémie 10.13 Ezéchiel 34.26 Esaïe 44.3 Jérémie 14.22 Jacques 5.7
2 Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.Ezéchiel 34.5 Osée 3.4 Matthieu 9.36 Jérémie 27.9 Genèse 31.19
3 Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.Ezéchiel 34.16-34.17 Sophonie 2.7 Esaïe 10.12 Esaïe 56.9-56.12 Esaïe 24.21
4 Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila mtawala pamoja.Zacharie 9.10 Nombres 24.17 Zacharie 9.8 Esaïe 22.23-22.25 Psaumes 118.22
5 Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.Aggée 2.22 Psaumes 20.7 Zacharie 14.13 Psaumes 18.42 Joël 3.12-3.17
6 Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia.Zacharie 13.9 Zacharie 10.12 Jérémie 3.18 Esaïe 14.1 Jérémie 31.1
7 Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana.Zacharie 9.15 Esaïe 38.19 1 Pierre 1.8 Genèse 18.19 Genèse 43.34
8 Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka.Esaïe 5.26 Jérémie 33.22 Esaïe 7.18 Jérémie 31.10-31.11 Ezéchiel 36.10-36.11
9 Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi.Ezéchiel 6.9 1 Rois 8.47-8.48 Osée 2.23 Daniel 3.1-3.6 Michée 5.7
10 Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana.Osée 11.11 Michée 7.14 Jérémie 22.6 Ezéchiel 47.18-47.21 Esaïe 19.23-19.25
11 Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.Ezéchiel 30.13 2 Rois 2.14 Esaïe 19.5-19.7 Sophonie 2.13 Josué 3.15-3.17
12 Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina lake, asema Bwana.Michée 4.5 Zacharie 10.6 Psaumes 68.34-68.35 Esaïe 41.10 Ephésiens 6.10

Cette Bible est dans le domaine public.