Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 12.9
Bible en Swahili de l’est


1 Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.Osée 5.13 Jérémie 22.22 Osée 11.12 Job 15.2 Ezéchiel 17.10
2 Bwana naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.Osée 4.1 Michée 6.2 Jérémie 25.31 Esaïe 24.21 Galates 6.7
3 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;Genèse 25.26 Genèse 32.24-32.28 Romains 9.11 Jacques 5.16-5.18
4 Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;Genèse 35.15 Malachie 3.1 Actes 7.30-7.35 Genèse 32.9-32.12 Esaïe 63.9
5 Naam, Bwana, Mungu wa majeshi; Bwana ndilo kumbukumbu lake.Exode 3.15 Psaumes 135.13 Genèse 28.16 Esaïe 42.8 Genèse 32.30
6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.Michée 6.8 Osée 6.1-6.3 Zacharie 7.9 Joël 2.13 Osée 14.1
7 Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.Proverbes 11.1 Michée 2.1 1 Timothée 6.9-6.10 Jean 2.16 Amos 8.5-8.6
8 Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.Apocalypse 3.17 Psaumes 62.10 Zacharie 11.5 1 Timothée 6.17 Jérémie 2.23
9 Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.Lévitique 23.40-23.43 Néhémie 8.15-8.17 Osée 13.4 Esdras 3.4 Jérémie 35.7
10 Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.2 Rois 17.13 Ezéchiel 20.49 Joël 2.28 Ezéchiel 4.1-4.5 Ezéchiel 15.1-15.8
11 Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.Osée 6.8 Osée 4.15 Osée 8.11 Osée 9.15 Osée 10.1
12 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu, Na Israeli alitumika apate mke; Ili apate mke alichunga kondoo.Genèse 27.43 Genèse 29.18-29.28 Genèse 32.27-32.28 Deutéronome 26.5 Genèse 31.41
13 Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.Exode 12.50-12.51 Actes 3.22-3.23 Psaumes 77.20 Exode 13.3 Esaïe 63.11-63.14
14 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.Ezéchiel 18.13 Daniel 11.18 2 Rois 17.7-17.18 1 Samuel 2.30 Osée 7.16

Cette Bible est dans le domaine public.