Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 12.8
Bible en Swahili de l’est


1 Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.Jérémie 22.22 Osée 11.12 Osée 5.13 Esaïe 30.6-30.7 2 Rois 15.19
2 Bwana naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.Michée 6.2 Osée 4.1 Osée 4.9 Matthieu 16.27 Esaïe 8.7-8.8
3 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;Genèse 25.26 Genèse 32.24-32.28 Jacques 5.16-5.18 Romains 9.11
4 Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;Genèse 35.15 Genèse 32.29 Genèse 48.15 Psaumes 66.6 Hébreux 6.13-6.18
5 Naam, Bwana, Mungu wa majeshi; Bwana ndilo kumbukumbu lake.Exode 3.15 Esaïe 42.8 Genèse 32.30 Psaumes 135.13 Genèse 28.16
6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.Michée 6.8 Osée 14.1 Osée 6.1-6.3 Zacharie 7.9 Joël 2.13
7 Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.Proverbes 11.1 Michée 7.2 Michée 6.10-6.11 Ezéchiel 16.3 Proverbes 16.11
8 Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.Apocalypse 3.17 Psaumes 62.10 Zacharie 11.5 Malachie 3.13 Luc 10.29
9 Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.Lévitique 23.40-23.43 Néhémie 8.15-8.17 Osée 13.4 2 Samuel 7.2 Nombres 15.41
10 Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.2 Rois 17.13 Ezéchiel 20.49 Joël 2.28 Jérémie 25.4 Jérémie 19.10
11 Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.Osée 8.11 Osée 6.8 Osée 4.15 Osée 9.15 Osée 10.1
12 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu, Na Israeli alitumika apate mke; Ili apate mke alichunga kondoo.Genèse 27.43 Genèse 29.18-29.28 Genèse 31.41 Genèse 28.1-28.22 Genèse 32.27-32.28
13 Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.Psaumes 77.20 Exode 13.3 Esaïe 63.11-63.14 Exode 12.50-12.51 Actes 3.22-3.23
14 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.Daniel 11.18 Ezéchiel 18.13 2 Rois 17.7-17.18 Ezéchiel 24.7-24.8 2 Samuel 1.16

Cette Bible est dans le domaine public.