Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 45.2
Bible en Swahili de l’est


Sort de Baruc

1 Neno hili ndilo ambalo Yeremia, nabii, alimwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu kwa kinywa cha Yeremia, mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema,
Jérémie 36.1 Jérémie 36.4 Jérémie 32.12 Jérémie 36.32 Jérémie 25.1
2 Bwana, Mungu wa Israeli, akuambia wewe Ee Baruku;
Hébreux 2.18 2 Corinthiens 7.6 2 Corinthiens 1.4 Esaïe 63.9 Hébreux 4.15
3 Ulisema, Ole wangu! Kwa maana Bwana ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha.
Galates 6.9 2 Corinthiens 4.1 2 Corinthiens 4.16 Lamentations 1.13 Psaumes 42.7
4 Basi, mwambie hivi, Bwana asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang’oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.
Jérémie 18.7-18.10 Jérémie 31.28 Jérémie 1.10 Psaumes 80.8-80.16 Genèse 6.6-6.7
5 Je! Unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema Bwana; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.
Jérémie 39.18 Jérémie 21.9 Romains 12.16 Jérémie 38.2 Jérémie 25.26

Cette Bible est dans le domaine public.