Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 93
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Psaumes 96.10 Psaumes 65.6 Psaumes 97.1 1 Chroniques 29.12 Esaïe 45.18
2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele. Psaumes 45.6 Psaumes 90.2 Apocalypse 2.8 Psaumes 145.13 Apocalypse 1.17-1.18
3 Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake. Psaumes 96.11 Psaumes 18.4 Psaumes 69.1-69.2 Apocalypse 12.15 Esaïe 17.12-17.13
4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu. Psaumes 65.7 Psaumes 89.6 Psaumes 89.9 Psaumes 114.3-114.5 Job 38.11
5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele. Lévitique 19.2 Psaumes 29.2 Lévitique 10.3 Psaumes 99.9 Apocalypse 21.27

Cette Bible est dans le domaine public.