Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 140.2
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.Psaumes 18.48 Psaumes 71.4 Psaumes 17.13 Psaumes 140.4 Habakuk 1.2-1.3
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.Psaumes 56.6 Psaumes 36.4 1 Samuel 24.11-24.12 Osée 7.6 Nahum 1.11
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao.Psaumes 58.4 Psaumes 57.4 Matthieu 12.34 Genèse 3.13 Psaumes 59.7
4 Ee Bwana, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.Psaumes 71.4 Proverbes 18.5 Psaumes 36.11 Psaumes 17.8-17.9 Psaumes 17.5
5 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.Psaumes 35.7 Psaumes 142.3 Jérémie 18.22 Psaumes 57.6 Psaumes 123.3-123.4
6 Nimemwambia Bwana, Ndiwe Mungu wangu; Ee Bwana, uisikie sauti ya dua zangu.Psaumes 16.2 Psaumes 31.14 Psaumes 142.5 Lamentations 3.24 Psaumes 91.2
7 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita.Psaumes 144.10 Psaumes 28.7-28.8 Psaumes 62.7 2 Samuel 8.14 Psaumes 18.35
8 Ee Bwana, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.Deutéronome 32.27 Psaumes 27.12 Job 5.12-5.13 Psaumes 10.2-10.3 Psaumes 94.20-94.21
9 Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike.Psaumes 7.16 Proverbes 18.7 Proverbes 12.13 Esther 7.10 Proverbes 10.11
10 Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.Psaumes 11.6 Psaumes 21.9 Matthieu 13.50 Apocalypse 21.8 Exode 9.23-9.24
11 Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.Psaumes 34.21 Psaumes 12.3-12.4 Proverbes 17.20 Esaïe 3.11 Proverbes 18.21
12 Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.Psaumes 9.4 1 Rois 8.49 1 Rois 8.45 Psaumes 72.12-72.14 Proverbes 22.22
13 Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.Psaumes 11.7 Psaumes 16.11 Psaumes 23.6 Psaumes 73.24 Jean 14.3

Cette Bible est dans le domaine public.