1  Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. 
Esaïe 57.1  Esaïe 59.13-59.15  Esaïe 1.21-1.22  Esaïe 59.4  Genèse 6.12  
 2  Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; 
Romains 16.18  Psaumes 41.6  Jérémie 9.8  Psaumes 10.7  Psaumes 144.8  
 3  Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi; 
Apocalypse 13.5  Daniel 7.8  Daniel 4.30-4.31  Proverbes 18.21  Psaumes 17.10  
 4  Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? 
Jacques 3.5-3.6  Jérémie 2.31  Jérémie 18.18  Genèse 3.5  2 Thessaloniciens 2.4  
 5  Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. 
Proverbes 14.31  Esaïe 33.10  Job 5.21  Juges 10.16  Psaumes 146.7-146.8  
 6  Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. 
Proverbes 30.5  Psaumes 18.30  Psaumes 19.8  2 Samuel 22.31  Psaumes 119.140  
 7  Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. 
1 Pierre 1.5  Psaumes 37.28  Deutéronome 33.3  Psaumes 10.18  Esaïe 27.3  
 8  Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu. 
Juges 9.18-9.57  Michée 6.16  Proverbes 29.12  Job 30.8  Osée 5.11