Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 11.7
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?Psaumes 56.11 1 Samuel 23.14 Psaumes 25.2 Psaumes 7.1 1 Samuel 20.38
2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.Psaumes 21.12 Jérémie 9.3 Psaumes 37.14 Psaumes 7.10 Psaumes 94.15
3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?Psaumes 82.5 2 Timothée 2.19 Actes 4.24-4.33 Esaïe 58.12 Daniel 3.15-3.18
4 Bwana yu katika hekalu lake takatifu. Bwana ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu.Psaumes 18.6 Psaumes 103.19 Esaïe 66.1 Habakuk 2.20 Matthieu 5.34
5 Bwana humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.Jacques 1.12 Genèse 22.1 Zacharie 11.8 Psaumes 17.3 1 Pierre 1.7
6 Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao.Ezéchiel 38.22 Genèse 19.24 Psaumes 75.8 Job 18.15 Esaïe 24.17-24.18
7 Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.Psaumes 45.7 Psaumes 17.15 Psaumes 33.5 Job 36.7 Psaumes 7.9

Cette Bible est dans le domaine public.